Sera ya Faragha
Ilisasishwa mwisho: Machi 2025
Ankaara inajali faragha yako. Sera hii ya faragha inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa zako za kibinafsi.
Taarifa tunazokusanya
Tunakusanya jina, barua pepe, nambari ya simu (hiari), maelezo ya biashara, wateja, bidhaa/huduma, mauzo, ankara na quotations unazoongeza kwenye mfumo.
Jinsi tunavyotumia taarifa
Tunatumia taarifa zako kuendesha akaunti yako, kuonyesha sales, inventory, wateja, ankara na ripoti, na kuboresha jukwaa. Tunaweza kutumia barua pepe au simu kwa arifa muhimu kuhusu akaunti na huduma zetu.
Kushiriki taarifa
Hatushiriki taarifa zako za kibinafsi na watu wa nje kwa madhumuni ya matangazo. Taarifa za ankara au quotation zinaweza kuonekana kwa mteja pale unapotuma au kushiriki hati hiyo - ni sehemu ya huduma.
Usalama
Tunachukua hatua za kiusalama kulinda data yako (mfumo wa usimbaji fiche, idadi ndogo ya watumiaji wenye ruhusa). Unapaswa kuweka nenosiri lako kwa usalama na kutuarifu mara moja ikiwa una mashaka kuhusu akaunti yako.
Haki zako
Unaweza kufikia na kusahihisha taarifa zako za wasifu kutoka kwenye Mipangilio. Unaweza kutuomba kufuta akaunti na data yako kwa kushughulikia msaada.
Mabadiliko
Tunaweza kusasisha sera hii ya faragha. Tutawataarifa watumiaji kuhusu mabadiliko muhimu. Kuendelea kutumia jukwaa kunamaanisha unakubali sera iliyosasishwa.
Wasiliana nasi
Ikiwa una maswali kuhusu sera hii ya faragha, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe ya msaada.
Wasiliana na Msaada